Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 24, 2013

Lipumba aonya aonya mikataba ya siri na China


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ameonya tabia ya kuingia mikataba yenye mazingira ya siri na makampuni kutoka nchini China, kuwa inaweza kuendelea kulitia aibu Taifa. Alitolea mfano aibu iliyoikumba nchi kutokana na usiri huo huo kuwa ni mkataba kati Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya China Communications Construction Company (CCCC). Kwa mujibu wa Lipumba, aibu hiyo ilimfanya Rais Jakaya Kikwete, alazimike kuvunja Baraza la Mawaziri kutokana na kashfa iliyokuwa ikiwakabili mawaziri wake. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu ujio wa Rais wa China, Xi Jinping, anayewasili leo, Prof. Lipumba ambaye pia ni Mtaalamu wa Uchumi, alisema ni wazi Tanzania imekuwa ikijikuta katika aibu kutokana na usiri huo wa mikataba ya miradi ya maendeleo inayoiingia na wawekezaji wa makampuni kutoka China.

Profesa Lipumba, alisema ziara hiyo ya Rais wa China inatakiwa kutumiwa kama fursa ya pekee kwa Taifa na isiwe majuto kwa Watanzania ambao kila siku wamekuwa wakiwashangilia wawekezaji ambao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria. “Ukweli ulio wazi katika nchi nyingi za Afrika kumekuwa na manung’uniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika, ikiwemo makampuni kutoka China, yanayowekeza katika katika sekta ya madini na yale yanayoshiriki katika ujenzi wa miundombinu, hasa ya barabara.

“Hivi karibuni nchi yetu ilishuhudia aibu kwa waliokuwa waziri wa Uchukuzi na Naibu wake kulumbana hadharani kuhusu ujenzi wa gati namba 3. Ni wazi ziara hii ya Rais Xi Jinping tunajua kuna mikataba zaidi ya 17 ambayo itasainiwa mbele yake pamoja na Rais Jakaya Kikwete,” alisema Profesa Lipumba. Kwa mwenendo huo pamoja na malalamiko ya Watanzania, Prof. Lipumba alisema ni muhimu kwa mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje, kufanya uhakiki wa kina kuhusu kampuni zinazopewa kutekeleza miradi ya maendeleo.


Source: Kimwanga B. (March 2013) Lipumba aonya mikataba ya siri na China. Retrieved from Mtanzania

No comments: