Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, March 15, 2013

Kigogo wa CCM aishukia serikali kujeruhiwa Kibanda


Dk. Raphael Chegeni
MWENYEKITI wa zamani wa mabunge ya Maziwa Makuu (Amani Forum), Dk. Raphael Chegeni amesema kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda ni matokeo ya serikali kushindwa kuwajibika. Chegeni alisema kitendo cha serikali kupitia idara zake za usalama kusuasua kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaojihusisha na uhalifu, kimechochea uvunjifu wa amani. Alisema kutekwa kwa Kibanda na kukamatwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari, ni matukio ambayo yameanza kulitia doa taifa, na kuzua hofu kubwa kwa Watanzania. Dk. Chegeni ameyasema hayo jana wakati alipotakiwa kutoa maoni yake na Tanzania Daima Jumamosi kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoonekana hivi sasa hapa nchini, likiwemo tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Kibanda.

Alisema haamini kama Jeshi la Polisi na idara zingine za usalama zimeshindwa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola watu wanaojihusisha na uhalifu kama huo kwa raia wa kawaida, tofauti inavyotukia kwa viongozi wa serikali ambapo hufanya kazi kwa umakini. Dk. Chegeni ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), na mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu, alisema alipouawa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, RPC Liberatus Lyimo Barlow mwaka jana, polisi walikamata wahusika ndani ya muda mfupi. Alionya kwamba iwapo serikali haitachukuwa hatua za haraka kudhibiti uharamia huo kwa waandishi wa habari na watu wengine, sura na sifa njema ya Tanzania itaharibika mbele ya uso wa dunia, na kuitaka iwajibike kikamilifu kuwalinda raia wake na mali zao kwa hali ya juu. “Matukio ya namna hii yasipodhibitiwa, tasnia ya habari itadhoofika. Amani ni kitu muhimu sana, na lazima ilindwe kwa nguvu zote vinginevyo sifa ya nchi yetu itaharibika sana,” alisema.
Tukio la kutekwa na kujeruhiwa vibaya kwa Kibanda linafananishwa na matukio mengine likiwemo la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka.

Sourece: Sitta T. (March 16, 2013). Kigogo CCM aishukia serikali kujeruhiwa Kibanda. Mwanza. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: