Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, March 21, 2013

Kasi ya Mnyika yamtisha JK

KASI ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kushikia bango tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es Salaam, ni wazi jana ilionekana kumshutua Rais Jakaya Kikwete. Kwa muda mrefu sasa, Mnyika amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuhusu maji na hata wiki iliyopita aliitisha maandamano ya amani kwenda Wizara ya Maji, ili kumshinikiza kero za wananchi wa jimbo lake zisikilizwe.

Rais Kikwete, alionekana wazi kushutushwa na tatizo la maji na kutoa maagizo mazito kwa uongozi wa Wizara ya Maji, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, DAWASCO, wabunge na mkuu wa wilaya Kinondoni, wahakikishe Jumatatu ya wiki ijayo wanakutana naye Ikulu, kwa ajili ya kupanga mikakati ya kumaliza tatizo hilo.
 
Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana, alipokwenda kukabidhi kituo cha kisasa cha polisi, nyumba za askari polisi na kufungua Shule ya Msingi Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Baada ya kusikiliza kero ya maji, Rais Kikwete aliwaita viongozi wa Manispaa ya Kinondoni, akiwamo Kaimu Mkurugenzi, Godfrey Mugomi na kuwahoji ni lini watamaliza tatizo la maji.

Lakini katika hali ya kushangaza, viongozi hao walishindwa kueleza mikakati yao. Hali hiyo ilionekana kumshutua na kuamua kutoa maagizo ya kuwataka wafike Ikulu Jumatatu ijayo.

“Wananchi wa Kinondoni naomba msiandamane kudai maji, nimebaini tatizo liko wapi, nawaagiza viongozi wote waje ofisini kwangu Jumatatu wanieleze mipango yao,” alisema Rais Kikwete. Pia Rais Kikwete, ameagiza kujengwa kwa bomba kutoka Ruvu Juu na Chini, ambalo litahudumia wananchi wa Dar es Salaam mbali ya miundombinu iliyopo sasa ambayo alidai imejaa udanganyifu na wizi wa maji njiani. Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliagiza halmashauri ya Kinondoni kukutana na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haraka, kwa ajili ya kutafuta fedha katika vitega uchumi na kulipa fidia ya nyumba nne zilizopo karibu na daraja la Golani, ili kuondoa kona kali iliyopo.

CCM, CHADEMA

Katika ziara hiyo, wafuasi wa CCM na CHADEMA waliokuwa wamejipanga kando kando mwa barabara, walionekana wazi kutunishiana misuli. Wafuasi wao, waliokuwa wamevalia fulana, kofia na bendera na kuelekea kwenye daraja la Golani, inalotenganisha Kata ya Kimara Suka na Saranga, lilionekana wazi kuibua hisia kali mbele ya Rais Kikwete. Kabla ya kuwasili Rais Kikwete, wafuasi hao walionekana kurushiana maneno ya chini chini, huku wote wakitaka kupeperusha bendera zao.

Kutokana na hali hiyo, hali ya usalama katika eneo hilo ilianza kupotea kitendo ambacho Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Jordan Rugimbana na polisi kuingilia kati na kuwasuluhisha.  Wakati Rais Kikwete, akisaini kitabu cha wageni, tafrani ilizuka karibu na jukwaa kuu, baada ya wafuasi wa CCM kutaka kuondoa viti vya madiwani wa CHADEMA. Hata hivyo, wakati wa utambulisho shangwe zilizizima pale walipokuwa wakiwataja viongozi wa Chadema, akiwamo Mnyika na madiwani wa CHADEMA.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa kila kaya kwa wananchi waliohamishiwa Mabwepande. Nayo Kampuni ya Home Shooping Centre, waliahidi kutoa mabati 30 kwa kila kaya, ambao ni wadhamini wa ujenzi wa makazi ya wakazi wa Mabwepande.



 
Source: Masese B. (March 2013). Kasi ya Mnyika yamtisha JK. Retrieved from Mtanzania

No comments: