Mh Rais Nakusalimu,
Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia
ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo
ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini
katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua
mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku
hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma . Mh Rais katika waraka hule nilisema hivi “ Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile
nilichosema katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea katika Taifa lako na
langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo kidogo sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi
mwako kwani hali ya Nchi sio nzuri hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na upendo sasa
wanaanza kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.
Mh Rais, Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama vya upinzani na
yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na mkakati huo unaendelea dhidi ya Chadema
lakini kinachosikitisha ni kuwa wale waliobuni mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara
yake mbele .
Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na Ukanda hauishi tu kuangamiza hicho
Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa Ujumla , Mtu anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha
Wakristo kimsingi matamshi hayo hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya
Udini wao na na kufanya Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na hivyo mpango huo unafanya
Watu waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila na matokeo yake ndiyo haya tunaanza kuyaona leo .
Mh Rais, Taifa linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita kwenye mgogoro wa Waisilamu na
Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye vyombo vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa
busara zile zilizokuwa zimejaa hofu kubwa . Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu
anayepaswa kuchinja?
Mh Rais , Nilipoona jambo hili nilianza kujiuliza maswali mengi sana, kwanza , umakini huu kwa pande
zote mbili juu ya jambo hili umeletwa na nini na nani? Kwani yako mambo mengi yaliyokatazwa na Biblia
na Msaafu ambayo watu wote wa dini hizi mbili wamekataa kuyatii au kuyafuata , kwa mfano waislamu
na wakristo vijana kwa wazee wanakunywa pombe pamoja baadhi yao kujenga mahusiano hata ya
kimapenzi yasiyo rasmi bila hata kufuata utaratibu wa Msaafu wala Biblia lakini hapa hutaona ugomvi
mkubwa sana japokuwa ni masuala yanayo mkera na kumuudhi mwenyezi Mungu sana.
Mh Rais , ndio maana katika suala hili la nani achinje kati ya Muislamu na Mkristo niliposikia maafa yake
nikakumbuka waraka niliokuandikia mwaka jana kuhusu choko choko za Udini ambazo zimeanza
kuleta maafa ambazo Mwanzilishi wake ni CCM .
Mh Rais Chama chako unachokiongoza , Team yako imekuwa ikifanya sana propaganda hizi za, Udini ,
Ukabila , na Ukanda usiku na mchana , lakini nimekuwa nikikerwa sana na Jinsi kabila la Wachaga
linavyochukuliwa katika propaganda hizi na wanaofanya hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga
na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao wenyewe ni familia
moja ?
Kwa mfano , Mh Mwigulu Nchemba , Mh David Mathayo , Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa ,
Mh Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu Lipumba , Pro Mahalu ,
Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh Sospeter Muhongo , Mh Jaji Warioba, Idd Simba, Mh
Salmin Amour , na wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro . Sasa unajiuliza hawa wote ni
Viongozi ndani ya CCM na wengine ndio mabingwa wa kufanya Siasa za Udini na Ukanda , je wake zao ndani ya nyumba wanajisikiaje wanapoona waume zao wanatukana kabila za ndugu zao kwa sababu
ya Siasa ? Hii ni hatari kubwa Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na
pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa
Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara
inayozidi imani, lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama
wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo
liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo
kwa wengine lina sura ya Imani.
Nini Kifanyike?
Kwanza Chama chako na Viongozi wake uwakanye na kuwashauri mara moja kabisa kuacha propaganda
za udini na ukanda , kwani katika hili hakuna namna Nchi inaweza kubaki salama , kwani hizo choko
choko hazitokani na nia mbaya ya Waislamu na Wakristo bali ni siasa chafu iliyopandikizwa ili
kuangamiza vyama vya Siasa na sasa imekwenda zaidi na imeanza kuwatesa wakati ambao Nchi ina
matatizo mengi , Kwa mfano Chadema tulipoandama Arusha kupinga Uchaguzi wa Meya feki , Kiongozi mmoja wa Mkoa wa CCM hapa Arusha , alinukuliwa na vyombo vya habari akidai tunafanya
maandamano hayo kwa sababu za Udini na ndio maana hatumtaki Meya , lakini kitu cha kushangaza
huyu Meya Feki ni Mkristo tena Mchaga Kabila langu , lakini niliambiwa na tunampinga na Maaskofu
wanampinga kwa sababu Chadema ni Chama cha Udini ‘ sasa najiuliza kama Meya huyu Feki ni Mchaga
na ni Mkristo je hayo madai ya kijinga yanatoka wapi ? Kama Ukristo ni ajenda kubwa kwetu kwani nini tulimpinga sasa ? Huu ni mfano mmoja iko mingi sana inayoashiria mkakati wa makusudi wa
kuangamiza Chadema na huku mkisahau kuwa maliangamiza Taifa , na ndio Mkuu wa Mkoa wa Arusha
alipokuja tu alidai kuwa amekuja kupambana na Chadema na Wachaga , ila nimuhakikishie hataweza na
asijaribu kamwe na mikutano ambayo amekuwa akiifanya aiche mara moja .
Pili, Mh Rais, ninaamini kuwa wewe umesafiri Nchi mbali mbali kuliko mimi , Ukienda Marekani , Spain ,
Brazil , China , Hong Kong , UK, Italy , Sweden, Botswana , Namibia , South Afrika , Zimbabwe na Nchi
nyiongi utaona Maduka au Mabucha ya Nyama yameandikwa (Halal ) au unanua bidhaa yeyote ya aina
ya Nyama na kukuta imeandikwa “Halal” na ni ustarabu kwamba bidhaa hiyo machinjio yake
yamezingatia maadili ya Dini ya Kiislamu na Waislamu wenye Imani thabiti na Imani yao hapo ndipo
watakapofanya manunuzi yao katika bidhaa hiyo ya aina ya Nyama. Lakini maeneno hayo hayo unaweza kupata nyama katika maduka mbali mbali yasiozingatia utaratibu huo na kwa hivyo watu wasiojali sana
masuala ya Imani wala hawatasumbuka kuuliza na kusoma kama Nyama hiyo imezingatia masuala ya
matakwa ya Imani Fulani.
Hivyo, Mh Rais, nafikiri ni vyema utaratibu huu ukaletwa hapa kwetu ili tuonyeshe Kujali Imani ya
Waislamu katika Jambo hili ambalo limekuwa kwazo katika Jamii hizi mbili kubwa na kama ufumbuzi
wake hautakuwa kuzingatia hili basi tarajia uchungu kuendelea kutembea kwenye vifua vya watu bila
kusema na siku moja hali inaweza kuwa mbaya na tukapoteza Taifa. Mh Rais, naiona hofu isiyokuwa ya kweli ya Mh Waziri Mkuu kuwa tukiruhusu hilo kuwa Wakristo na
Waislamu wataweza kutengana kwenye mambo mengine mengi haswa katika Biashara na mambo
mengine , kitu ambacho nasema sio kweli kwani , Sukari ,Mchele , Soda na Juisi na bidhaa nyingi hazina
makatazo na maelekezo katika Imani , Mfano kila Mkristo anajua kuwa Mwislamu hatumi Nguruwe na
Nguruwe kwa mwislamu ni haramu na hivyo Mkristo hawezi kupika Nguruwe na huku akijua kuwa
wageni wake siku hiyo ni Waislamu.
Kwa hiyo hofu ya kuligawa Taifa kwa kurusu jambo hili haliwezi kutokea kwani ni miiko ya Kiimani
ambayo pande zote zinapaswa kuheshimiana ili upande mmoja usione umekandamizwa na kupuuzwa ,
na hofu ya kibiashara inayoweza kutokea katika suala hili inapaswa kupuuzwa kwani IMANI ni zaidi ya
Biashara japokuwa sioni jambo hili likitokea . Mh Rais, nisikuchoshe sana, lakini haya ni maoni yangu na Mke wangu na sio Chama changu tumeamka
leo Asubuhi tukasema tukuandikie tena kwani wewe ni Mkuu wa Nchi , Najua unaweza kuwa busy sana
kusoma waraka huu mrefu ila najua Mwigulu na Nape lazima wausome na Rizwan pia hivyo niwaombe
wakufikishe ujumbe huu kwa niaba ya familia yangu. Mh Rais , We are pressed on every side by troubles, but not crushed and broken. We are perplexed
because we don,t know why things happen as they do . But we don’t give up and quit, we are hunted
down BUT God never abandons Us, We get knocked down BUT we get up again and keep going. The
root of life need commitment and there’s a lot of suffer to get at the Climax. Don’t Give Up Mr
President please, Help our Country now.
Godbless Jonathan Lema
No comments:
Post a Comment