Mwanachama mpya wa CCM Juliana Shonza amekiri kuwa CHADEMA wako imara na waliojipanga ipasavyo. Shonza alikuwa akichangia katika kikao cha kichama kilichofanyika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba,jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa kikizungumzia,pamoja na mambo mengine,jinsi mikutano iliyofanywa na CCM hivi karibuni ilivyokiimarisha chama.
'CHADEMA wako imara;wamejipanga. Kuwatikisa nikazi kubwa. Kila mtu hapa ni shahidi kuwa chama chetu(CCM) kinafanya kila juhudi kuimaliza CHADEMA. Kazi hiyo ilianza siku nyingi. Tumefanya kila tuwezalo kufanikisha hilo lakini haikuwa kazi rahisi.' alisema Shonza akionesha hofu ya kutofanikiwa.
'Hivisasa CHADEMA wamepandikiza watu wao hadi Usalama wa Taifa na hata humu ndani wamo CHADEMA-damu. Huo ndio uimara ninaouzungumzia. Wanalindwa kila idara na kupata habari yoyote waitakayo.Wnapata kila hatua inayopigwa na CCM na vyama vingine.Lazima juhudi ziongezwe.Cha kufurahisha ni kuwa tupo vijana wengi watiifu kwa CCM hadi kufanikishwa kazi ya kuidhoofisha CHADEMA.' aliongeza akisindikizwa na mchanganyiko wa makofi na miguno.
Kama hivyo ndivyo,hongereni sana CHADEMA.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
Source: Vuta Nkuvute (February 28, 2013). Shonza: CHADEMA wako imara. Retrieved from Jamiiforums
No comments:
Post a Comment