KAMANDA MBOWE KUONGOZA MASHAMBULIZI
Joto la kisiasa katika nyanda za juu kusini linaelekea kufika nyuzi ridi 100.Hii ni tathmini iliyofanywa katika mikoa minne inayounda eneo hili ambayo ni Mbeya,Njombe,Iringa na Ruvuma.Mara tu baada ya kutangazwa kwa tarehe ya uzinduzi rasmi wa kanda ambao utafanyika tarehe 27.2.2013,kumekuwa na pilika pilika nyingi kwa maeneo yote ili kuhakikisha kuwa mambo ya uzinduzi unafanyika kwa kiwango cha juu kushinda Arusha na Mwanza ambako tayari uzinduzi ulifanyika siku chache zilizopita.Pamoja na kuhudhuriwa na maelfu ya watu katika maeneo ambayo tayari uzinduzi umefanyika; watu wa kanda hii wamejipanga kuvunja rekodi. uzinduzi huo utafanyika katika jiji la Mbeya.
Kwa taarifa za uhakika toka mikoa husika,mkoa wa Njombe ambako ni makao makuu ya jimbo(kanda) hadi tarehe 22.2.2013 tayari michango iliyochangwa kwaajili ya uzinduzi ilikuwa ni mikubwa sana.Kama ni mahindi tungesema tayari gunia la kumi lililojaa fedha na kushonwa vilivyo.Pia kulikuwa na magari yaliyoandaliwa zaidi ya 123 yatakayoelekea kwenye uzinduzi huko Mbeya. Pia kutoka Iringa na Ruvuma kuna taarifa zinazoashiria maelfu ya watu kujiandaa tayari kwa safari ya kwenda Mbeya kushiriki uzinduzi utakaofanywa na kamanda wa anga Mhe.Mbowe. Kwa vyovyote vile msafara utakaoanzia Makambako(makao makuu ya Gavana mtarajiwa) utakuwa ni mkubwa na naamini kwa hapa Tanzania itakuwa ni mara ya kwanza kushuhudia msafara mrefu wa magari na pikipiki.
Source: Lutondwe (Februeary 23, 2013) Maandalizi ya uzinduzi kanda (CHADEMA) yavunja rekodi. Retrieved from Jamii Forums, the home of great thinkers.
No comments:
Post a Comment