Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, January 28, 2013

GAVANA: KATIBA IWABANE WANAOFICHA FEDHA NJE


GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Benno Ndullu, amependekeza katika Katiba mpya ijayo kiwekwe kipengele cha sheria kitakachowabana watakatishaji fedha pamoja na wale wanaozificha kwenye mabenki ya nchi za nje.

Prof. Ndullu, alitoa kauli hiyo jana baada ya kuwasilisha mapendekezo ya taasisi hiyo nyeti mbele ya tume ya kukusanya maoni ya mabadiliko ya Katiba mpya jijini Dar es Salaam. “Kihistoria mtu alikuwa akipeleka fedha zake nje ikiwa anazo nyingi tofauti na sasa ambapo watu wachache wameharibu utaratibu wa kuiba na kwenda kuzificha nje,” alisema.

Alifafanua kuwa watu kwa kiwango kidogo wameiamini nchi yao na wameanza kuzihifadhi fedha nyingi hapa nchini na kwamba fedha zilizopo hadi wakati huu ni kama dola bilioni 2.2 bila kuhesabu zile zilizoko nje ya nchi. Pia alisema kuwa sheria za msingi za kuilinda BoT zikiwekwa zitasaidia kutoa huduma nyeti na za kiuchumi kwa wananchi wake na itakuwa na uhuru wa kushughulikia masuala yanayoihusu kuhusu fedha.

Akizungumzia suala la siasa kuingizwa katika benki hiyo, Ndullu alisema amependekeza kuwa siasa ibaki kama siasa na BoT ibaki na majukumu yake bila kuingiliwa kwani ina mambo muhimu ya kufanya hivyo inapaswa kuwa na uhuru.

Gavana aliongeza kuwa amependekeza ziwekwe sheria mama kwenye Bunge za kuikinga BoT kufanya mambo yake yenyewe pasipo kuingiliwa ili kuboresha utendaji kazi. Kuhusu suala la kutakatisha fedha, Prof. Ndullu alisema hawezi kulizungumzia sana lakini anafikiri hizo sheria anazozisema ikiwa zitawekwa kwenye Katiba mpya zitaweza kuainisha suala hilo.


Mnale, H.  ( January 29, 2013). Tanzania Daima, Sauti ya Watu.


No comments: