Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, November 5, 2015

ASANTENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI, MBARALI 2015


Kwa marafiki na wapenzi wangu wote tulio shirikiana kwenye kampeni zangu, Liberatus Mwang’ombe, za ubunge 2015 jimbo la Mbarali;



Kwanza kabisa naomba samahani kwa kuchelewa kuwashukuru wote mlio tumia muda wenu, mali zenu, na nguvu zenu kwenye kampeni hizi.  Nawashukuru kwa kunipa support ya kifedha, mawazo, vyombo, ushirikiano usio na kikomo; na kuniamini.

Natambua wazi tumepita kwenye kampeni ambazo ni ngumu na zenye changamoto nyingi, lakini hata siku moja hamkuweza kuniacha. Tulilia pamoja, tulicheka pamoja na tulifurahi pamoja na tuli huzunika pamoja.  Kuna siku zilipita bila hata kupata chakula cha mchana; lakini, kwa sababu lengo letu lilikuwa ni moja, hatukuteteleka.  Mwisho wa siku tumemaliza kampeni salama kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.

Kwa umoja wetu tumeweza kuionyesha Mbarali, Tanzania na dunia kuwa tukiungana na kuamua kufanya kitu hakuna wa kutuzuia.  Tumefanikiwa kwa kuweza kufikia kata zote 20; na kufanikiwa kupata madiwani 8 kutoka 2 tulio kuwa nao 2010.  Kwa pamoja tulishirikiana kwa nguvu zote na maarifa yote.

Hadi tunamaliza uchaguzi matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Haroon Mulla (CCM) 45,352
Liberatus Mwang'ombe (CHADEMA) 36,603
Modestus Kirufi (ACT) 20,606
Gamdust Hajji (CUF) 382
Getruda Pwilla (NCCR) 120
Nurdin (UPDP) 114

Siumii kunyang'anywa ushindi Mbarali. Naumia navyo ona wakina mama, vijana na wazee wa Mbarali walio jitolea kwa moyo moja bila kulipwa kufanikisha kampeni zetu wanavyo toa machozi na kuja nyumbani wakiniuliza haki yao ipo wapi. Tunaishi kwenye nchi ambayo hata ukipiga Kura; huna hakika kama itahesabiwa, na hata kama ikihesabiwa; huna hakika kama itaenda kwa yule uliye mpigia.

Tumemaliza kampeni na uchaguzi; najua inaumiza sana, lakini ni wakati wa kurudi kwenye maisha yetu ya kawadi na kuondoa makandokando na tofauti zilizo jitokeza kipindi cha kampeni.  Sisi wote ni wamoja na naamini hakuna ambaye aliingia kwenye kampeni kwa maslai binafsi; wote tulikuwa tunapigania maslai ya Mbarali na Tanzania yetu.

Assanteni sana kwa ushirikiano, umoja na mapenzi mliyo yaonyesha kipindi cha kampeni na sasa. Nisinge fikia hapa bila ya nyinyi, kwani ili niwe mimi ni lazima nyinyi muwepo; vinginevyo “I’m nothing”.

MUNGU IBARIKI MBARALI, MUNGU IBARIKI TANZANIA


Liberatus Laurent Mwang’ombe
BAGASA2015

UJASIRI WA KUAMUA/UJASIRI WA KUTHUBUTU

Thursday, October 22, 2015

BREAKING NEWS: MBIO ZA UBUNGE: MAFULIKO YAHAMIA MBARALI KWA MWANG'OMBE, AVUNJA REKODI

Liberatus Mwang'ombe "Libe" ameendelea kuvunja rekodi kwa kukusanya watu wengi kuliko mgombea yeyote wa ubunge aliye wahi kutokea jimbo la Mbarali. Mh. Mwang'ombe ambaye amekuwa akiendesha mikutano yake kwa namna ya kipekee kabisa; leo, baada ya kuhutubia aliacha dakika 45 ambapo alisema "nimeomba mdahalo na mgombea wa CCM, Haroon, amekataa; nimeomba mdahalo na mgombea wa ACT, Modestus Kilufi, amekataa; sasa nawaruhusu watu wa Ubaruku mnifanyie mdahalo peke yangu."
Watu wa Ubaruku walimuuliza Mh. Mwang'ombe maswali zaidi ya 10 ambapo walipata majibu stahiki hadi wananchi wakawa wanamwambia Mh. Mwang'ombe inatosha nenda kapumzike. Moja ya maswali aliyo ulizwa Mh. Mwang'ombe ni pamoja na nini atakifanya juu ya huduma ya afya. Mwang'ombe alisema atashirikiana na madiwani, bwana afya wa wilaya na madaktari kuhakikisha wana boresha huduma za afya Mbarali. Zaidi, Mh. Mwang'ombe anaamini kuwa huduma ya afya ni haki ya binadamu; hivyo basi, serikali inawajibu wa kuhakikisha inapeleka vifaa kama, madawa, gloves, nyembe, sindano kwenye vituo vya afya.


 Mh. Mwang'ombe akiendelea kutililika jukwaani

Ni nyomi
 Juu na chini: umati wa watu ulio jitokeza kumsikiliza Mh Liberatus Mwang'ombe


Wednesday, October 21, 2015

PICHA: JUST PICHA: MWANA DIASPORA NA MBIO ZA UBUNGE: WANAMWITA RAIS WA MBARALI

Ni Liberatus Mwang'ombe "Libe" aliye wahi kuishi Maryland, DC na Virginia (DMV) amekuwa akivunja rekodi kwenye historia za mbio za ubunge jimbo la Mbarali kwa kukusanya vijana na watu wa rika mbalimbali wengi kuliko ilivyo wahi tokea jimboni Mbarali. 



 Juu na chini: Libe katika ubora wake


 Juu na chini: George Tito aka Mbu Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Mbeya akimnadi Mh. Mwang'ombe

Tuesday, October 20, 2015

BREAKING NEWS: MBOWE: LIBERATUS MWANG'OMBE NDIYE MGOMBEA WA UBUNGE MBARALI KUPITIA UKAWA

Liberatus Mwang'ombe akichanganua changamoto za Mbarali mbele ya Mh. Lowassa
Mh. Mbowe "Liberatus Mwang'ombe ndio mgombea halali wa UKAWA- Mbarali"

 Juu; baaa ya chopa ya Mh. Lowassa kutua. Chini: Mh. Mwang'ombe akiwaongoza wageni jukwaani

Bango: Mbarali tunamtaka Mwang'ombe
 Wana Mbarali wamesema watamchagua Mh. Mwang'ombe

 Juu Mh. Kingunge akielezea kuwa mabadiliko hayazuiliki
 Meza kuu

Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

Friday, October 16, 2015

Liberatus Mwang'ombe aongelea changamoto za Mbarali na Mwananchi LTD




Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

BREAKING NEWS: MAMA REGINA LOWASSA USO KWA USO NA MWANA DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE

Mama Regina Lowassa leo alikuwa Chimala, Mbarali akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbarali, Liberatus Mwang'ombe "Libe". Akiongea na wana Mbarali mama Lowassa amesema mwang'ombe ni kijana mweledi, msomi, na mwenye maono na Mbarali; hivyo basi amewaomba wana Mbarali wasimpoteze Mh. Mwang'ombe. 

Mama Lowassa alishangazwa na umati uliojitokeza baada ya taarifa ya masaa matutu kuwa atasimama Chimala. Mh. Mwang'ombe akitoa shukrani zake kwa mama Lowassa kufika Mbarali alisema "Mbarali ina wapiga kura 143189 na watu wa Mbarali wameonyesha kila dalili ya kutaka mabadiliko". Mwang'ombe aliwaomba watu wa Mbarali wampeleke Dodoma akihutubia na kuwasisitiza wajitokeze kwa wingi Jumapili, tarehe 18/10/2015 saa 3 asubuhi ambapo Mh. Lowassa atakuwa anaunguruma naye. 

Mama Lowassa na Mh. Mwang'ombe katika ubora wao

 Mh. Mwang'ombe anakubalika Mbarali, hapa umati ukiwa umezingira gari lake lisiondoke
 Watu wa ,barali wanataka mabadiliko

Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

Tuesday, October 13, 2015

MBIO ZA UBUNGE: LIBERATUS MWANG'OMBE AENDELEA KUWA KIMEO KWA WAGOMBEA WENZAKE

Nyota ya mwana-diaspora kutoka Marekani inaonekana kung'aa kwenye mbio za ubunge mwaka huu. Ni Liberatus Mwang'ombe "Libe" ambaye amekuwa akijizolea umaarufu kila uchao. Mh. Mwang'ombe amekuwa akivunja rekodi kila siku kwa kuwa na mvuto kwenye mikutano yake kuliko mgombea yoyote aliye wahi kutokea kwenye historia ya jimbo la Mbarali.

Mh. Mwang'ombe anaye onekana kuwavutia watu wa rika mbalimbali amekuwa changamoto kwa wagombea wengine ambao kuna baadhi ya maeneo wameshindwa kufanya mikutano kwa kukosa watu na kuzomewa pale wanapo msema Mwang'ombe. Zaidi, mgombea wa ACT, Modestus Kilufi,  alikutana na dhahama baada ya kujaribu kumsema vibaya Mh. Mwang'ombe kwenye kijiji cha Chimala ambapo ndipo alipo zaliwa Mwang'ombe.  Mh. Kilufi alipo jaribu kuanza siasa za kumponda Mwang'ombe zilisikika sauti za watu wakipiga kelele na kusema kama unamsema huyo shuka jukwaani na ondoka. 

Baada ya kuona hasomeki,  Mh.Kilufi akabadilisha maneno na kuwaambia watu wa Chimala kuwa "kama hamta nipa kura mimi, msimpe Haroon (mgombea wa CCM), bora mpeni kijana Mwang'ombe". Baaada ya maneno hayo umati wa watu ulilipuka kwa shangwe




Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

DEVELOPING STORY: PICHA: MWANA DIASPORA BADO AENDELEA KUWA GUMZO MBIO ZA UBUNGE

Ni Liberatus Mwang'ombe ambaye amewahi kukaa Washigton D.C., ameendelea kukonga nyoyo za wana Mbarali kwa kila uchao. Kila baada ya mkutano wananchi wa Mbarali wamekuwa wakimuomba asipande gari na watembee naye umbali wa kilometer 2 hadi 3.

 "Wangapi watanipeleka Dododma? Mikono juu". Hayo yalikuwa maneno ya Mh. Mwang'ombe akiwauliza wananchi ambao wote walinyosha mikono juu
Baada ya mkutano mitaa ilifungwa na wananchi kumwambia Mh. Mwang'ombe asipande gari bali atembee nao umbali wa kilometer 2
 Juu na chini Mh. Mwang'ombe akiendlea kuuza ILANI ya chama chake.
 Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

 Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

Sunday, October 11, 2015

PICHA: JUST PICHA: KIJANA KUTOKA DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE AENDELEA KUCHANJA MBUGA MBIO ZA UBUNGE






Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574