Chama
cha Chadema kimezindua kampeni zake leo za uchaguzi wa udiwani kata ya iyela
kata hiyo imekuwa wazi bila diwani kwa muda wa miezi 5 sasa baada ya aliyekuwa
diwani mzee Mkwenzulu kufariki dunia mwanzoni mwaka huu. CHADEMA mgombea wao ni
Ndugu Charles Nkela na CCM mgombea wao ni mzee mmoja wa kihindi mwenye asili ya
Pakstan maarufu kama Chan Van Cheng ambaye naye atazindua kampeni zake zake
kesho jumamosi. CHADEMA walizindua kampeni kwa kuanza na maandamano makubwa
kabisa yaliyoshirikisha watu zaidi 2000 hivi yalianzia eneo la Air port na
kuishia uwanja wa soko la maendeleo katani hapo. Akizindua kampeni kiongozi
mmoja wa CHADEMA Ndg Mwampiki ambaye ni katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya Mbeya
mjini alisema kata hiyo ni tajiri kuliko zote jijini mbeya lakini kutokana na
usimamizi mbovu wa viongozi wa CCM watu wake wanaishi kimasikini kupita kawaida.
Kata
hiyo ndipo lilipo soko la sido la jijini Mbeya ina vyuo vikuu 2 kikiwemo Chuo
cha Teku na tia pia ina mabenki 5 na ndipo ulipo uwanja wa ndege wa jijini
Mbeya (sio songwe). Na barabara zake ni mbovu kuliko wakati kata ambaye yeye
Mh. Mwampiki ni diwani (mwakibete) haina vyote hivyo lakini ameisimamia vizuri
kiasi kufika mbali kwa kujenga shule ya Secondary yenye majengo 9 kwa
kuwachangisha wananchi wake sh.3000/=@ na chenji ikabaki wakati kata hiyo ya
Iyela diwani aliyepita alishindwa licha ya kuchangishi sh 10000/=@. Katika jiji
la Mbeya michango ya ujenzi wa shule za secondary ni sh 10000/= @kwa kata zenye
madiwani wa CCM na sh 3000/=@ kwa kata zenye madiwani wa CHADEMA ajabu ni kuwa
kata za CHADEMA zinakamilisha ujenzi haraka na chenji inabaki na za CCM licha
ya kuchangisha sh 10000/=@ zimeshindwa kukamilisha ujenzi huo na kukumbwa na
kashifa mbalimbali ikiwemo wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule mfano ni kata ya
Igawilo ambayo Mh.diwani wa kata hiyo ambaye pia ni naibu meya wa jiji la Mbeya
Ndg Chifoda Fungo alifikia kuiba hadi bati za shule ya kata yake ya
Mponja.
Hata
hivyo alifanya yote hayo na analindwa na mkuu wa wilaya ya mbeya mjini Ndg
Nolman Sigala inasemekana ni ndugu yake na wamesoma wote elimu ya secondary huko
bulongwa Makete. Wanambeya
kuweni makini chagueni mzalendo wa nchi hii na si wapenda ufisadi mkikosea
itawagharimu.
No comments:
Post a Comment