Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, May 18, 2013

CHADEMA kuzindua kampeni Manchira-Serengeti, Jumapili 19/05/2013


Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, kinatarajia kuzindua rasmi kampeni za kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Manchira. Uchaguzi huu unafuatia nafasi iliyokuwa wazi ambapo mgombea wa CCM Ndg. Mechama alifariki mwaka jana.

Uzinduzi wa Kampeni hizi, utaanza kwa maandamano makubwa kutoka Mugumu Mjini kuelekea Bwitengi. Habari za kuthibitika zinasema kwamba, kwa sasa Viongozi waandamizi wa CCM katika wilaya zote za Mkoa wa Mara wametia kambi Mugumu wakiweka mikakati yote halali na haramu, kuhakikisha mgombea wao anashinda. Kwa upande wa CHADEMA, mikakati mizito na makombora ya masafa mafupi na marefu, yanaandaliwa ili kuharibu na hatimaye kuwagaragaza CCM katika uchaguzi huu.

Kwa ufupi, Kata hii ya Manchira, ni moja kati ya kata 28 zinazounda wilaya na jimbo la Serengeti. Serengeti ni moja ya Wilaya tajiri zenye rasilmali nyingi huenda kuliko wilaya yoyote kanda ya ziwa. Na Kata hii ina eneo kubwa ambalo lina wawekezaji wa nje na ndani. Na hapa Manchira ndipo kuna bwawa kubwa la pekee ambalo linahudumia mji wa Mugumu kwa maji machafu kwa watu wachache, Lakini pia, pamoja na Bwawa hili kuwa kwenye Kata hii, wananchi wa Kata hii hawapati maji haya kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu!!

Hapa, nawaalika wapenzi wa CHADEMA, wana Serengeti, na wapenda mabadiliko, kuiunga mkono wa hali na mali ktk kuhakikisha Kata hii inakuwa chini ya CHADEMA

TANGAZO HILI LIMELETWA KWENU NA M/KITI WA FRIENDS OF CHADEMA SERENGETI

No comments: